![](https://ors-radio.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/picha.jpeg)
#Habari Katika kijiji cha Loswaki, kilichopo wilayani Simanjiro, ushiriki wa wanawake katika mikutano ya kijamii umeendelea kuwa mada ya mjadala wa maendeleo. Wanawake kama Winifrida Amos, mkazi wa kijiji hicho, wanasema kuwa kushiriki katika mikutano ni fursa ya kipekee ya kuhakikisha masuala yanayohusu wanawake yanajadiliwa ipasavyo na kupata ufumbuzi.
“Ninapenda kushiriki katika mikutano kwa sababu unakuta mambo yanayowahusu wanawake hayatetewi” anasema Winifrida. Hata hivyo, anasisitiza kuwa mila na desturi zisizofaa zinazomkandamiza mwanamke ni changamoto kubwa katika jamii ya Kimasai.
Changamoto za Ushiriki wa Wanawake
Moses Lukumay, Mwenyekiti wa kijiji cha Loswaki, anakiri kuwa ushiriki wa wanawake katika mikutano bado ni wa kiwango cha chini licha ya kuwepo kwa juhudi za kuhimiza wanawake kushiriki. Anasema kuwa wanawake wanaoshiriki, kama Winifrida Amos, mara nyingi wanatoa maoni yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya kijiji.
Kwa upande wake, Afisa Tarafa wa Terrat, Lekshon Kiruswa, anasema kuwa changamoto ya ushiriki wa wanawake haipo kijijini Loswaki pekee bali ni changamoto inayojitokeza katika tarafa nzima ya Terrat. Anasema jitihada za kuwahamasisha wanawake kushiriki katika mijadala ya kijamii zinaendelea kufanyika.
“Muamko wa wanawake kushiriki katika mijadala bado upo chini kwenye tarafa yetu” anasema Kiruswa.
Juhudi za Kukuza Ushiriki wa Wanawake
Ili kuboresha ushiriki wa wanawake, viongozi wa kijiji na tarafa wanapendekeza kuondoa vizuizi vya kijamii vinavyowazuia wanawake kushiriki kikamilifu, ikiwa ni pamoja na elimu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia na kuhamasisha jamii kuachana na mila kandamizi.
Makala mazuri Sanaa!! Especially katika muktadha wa jamii ya kimasai. Ors hakika ni radio ya jami