Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria ili kudhibiti ajali kutokana na ongezeko la wasafiri kipindi cha likizo za shule. Madereva wamehimizwa kuzingatia sheria za barabarani huku abiria wakitakiwa kununua tiketi kwenye ofisi rasmi ili kuepuka usumbufu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria kwa lengo la kudhibiti ajali, hasa katika kipindi hiki ambacho shule nyingi zimeanza kufungwa na kusababisha ongezeko kubwa la wasafiri, wakiwemo wanafunzi.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo uliofanyika katika stendi kuu ya mabasi jijini Arusha, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Zauda Mohamed amesema ongezeko la wasafiri katika kipindi hiki limeongeza hatari ya kutokea ajali hivyo ni muhimu kwa madereva kuwa makini zaidi.

SSP Zauda amewataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za barabarani na kuhakikisha magari yenye matatizo ya kiufundi yanawekwa pembeni ya barabara na kuweka alama ili kuepuka madhara kwa watumiaji wengine wa barabara.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Abiria Kanda ya Kaskazini, Bw. Godwin Mpinga ametoa wito kwa abiria kununua tiketi zao kwenye ofisi rasmi za mabasi husika ili kuepuka usumbufu na vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya mawakala wasio waaminifu.

Wakala wa mabasi ya abiria, Bw. Rashid Mohamed amesema ukaguzi huo umekuwa muhimu kwani umewasaidia kujifunza mambo mapya na kueleza changamoto wanazokabiliana nazo barabarani kwa lengo la kuzitatua ili kuboresha usalama wa usafiri.

Jeshi la Polisi limetoa ahadi ya kuendelea kufanya ukaguzi wa aina hii mara kwa mara ili kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa na ajali zinapungua kwa kiwango kikubwa.

Related Posts

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la madiwani jiji la Arusha limefungwa rasmi katika hafla ya kipekee iliyoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Mohamed Mchechengerwa.…

Continue reading
Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

World Sickle Cell Awareness Day ni siku inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Juni ili kuhamasisha elimu juu ya ugonjwa wa sikoseli. Ugonjwa huu wa damu, unaosababisha mabadiliko ya seli nyekundu…

Continue reading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa
Enable Notifications OK No thanks