
Kituo cha afya cha Mirerani kilichopo kata ya Endiamtu, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kinaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali licha ya jitihada zilizochukuliwa na serikali baada ya ripoti ya Orkonerei FM mwaka 2023.
Katika ripoti ya awali ya mwaka 2023, changamoto zilizobainishwa zilihusisha uhaba wa majengo, upungufu wa wahudumu wa afya, pamoja na ukosefu wa dawa na vifaa tiba. Hali hiyo ilisababisha madhara makubwa kwa jamii, ikiwemo ongezeko la maambukizi ya magonjwa kama kifua kikuu, na wagonjwa kulazwa sakafuni kutokana na uhaba wa vitanda.
Mabadiliko Yaliyojitokeza
Katika uchunguzi mpya wa mwaka huu, Orkonerei FM imetembelea tena kituo hicho na kubaini kuwepo kwa mabadiliko madogo yaliyofanyika, ikiwemo:
- Ujenzi wa chumba kipya cha mapokezi
- Uboreshaji wa jengo la kuhifadhia maiti
- Kuboresha eneo la utoaji wa dawa
Ili kufahamu zaidi sikiliza makala hii ya sauti na JOYCE ELIUS.