Kaya 22 Zenye Watu 96 Zapokelewa Rasmi Msomera Kutoka Ngorongoro

Jumla ya kaya 22 zenye watu 96 na mifugo 196 zilizohama kwa hiari kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro zimepokelewa rasmi katika Kijiji cha Msomera, Wilayani Handeni. Kaya hizo zimekabidhiwa makazi mapya, mashamba, na maeneo ya ufugaji kama ilivyoahidiwa na Serikali.

Akizungumza wakati wa mapokezi, Katibu Tarafa wa Sindeni, Bw. Baraka Nkatura, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi aliyekubali kuhama kwa hiari anapata huduma bora.
“Mtapatiwa nyumba za kisasa zilizojengwa kwenye maeneo yenye ukubwa wa ekari 2.5, mashamba ya ekari 5, na maeneo ya shughuli za ufugaji,” alisema Bw. Nkatura.

Miongoni mwa waliopokea nyumba mpya, Bw. Samweli Koromo alisema amefurahi kupewa nyumba bora na fursa za maendeleo ambazo hazikuwepo ndani ya hifadhi.
“Nimepata nyumba nzuri. Sasa nitaanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa ni msimu wa mvua,” alisema.

Kwa upande wake, Bi. Esther Naftal, mkazi wa Msomera aliyehama Ngorongoro miaka mitatu iliyopita, alisema maisha yao yamebadilika kwa ubora.
“Msomera tunalima, tunafanya biashara, watoto wanasoma, na maisha yameimarika. Wito wangu kwa waliobaki Ngorongoro ni waendelee kujiandikisha ili wanufaike na fursa hii,” alisema.

Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea kutoa elimu, kuandikisha, na kuhamisha wananchi wanaokubali kuhama kwa hiari. Ikielezwa kwamba wanaohama wanapewa uhuru wa kuchagua maeneo wanayotaka kuhamia huku Msomera ikiwa mojawapo ya maeneo yenye miundombinu bora.

Fuatilia @OrkonereiFM kwa habari zaidi kuhusu maendeleo ya zoezi hili.

Related Posts

TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

Serikali za vijiji katika Tarafa ya Terrat, wilayani Simanjiro, zimetakiwa kuwa na ushirikiano mzuri na wawekezaji waliopo kwenye maeneo yao kwa kuwaalika na kuwatembelea ili kujenga mahusiano mazuri na kushirikiana…

Continue reading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

Maji Safi na Salama ni Yapi?

Maji Safi na Salama ni Yapi?

Mbinu Bora za Uhifadhi wa Mazao ya Chakula kwa Usalama na Ufanisi

Mbinu Bora za Uhifadhi wa Mazao ya Chakula kwa Usalama na Ufanisi

Usalama wa Vijana Wanaochunga Mifugo Kwakuchinja

Usalama wa Vijana Wanaochunga Mifugo Kwakuchinja

Migogoro baina ya Wanyamapori na Binadamu Tanzania: Chanzo na Suluhisho

Migogoro baina ya Wanyamapori na Binadamu Tanzania: Chanzo na Suluhisho

Namna Shule ya Msingi Burunge Inavyonufaika na Uhifadhi wa Ushoroba wa Kwakuchinja

Namna Shule ya Msingi Burunge Inavyonufaika na Uhifadhi wa Ushoroba wa Kwakuchinja
Enable Notifications OK No thanks