![](https://ors-radio.co.tz/wp-content/uploads/2024/10/PICHA-1.jpg)
Na Mwandishi wetu.
Katika kijiji cha Sukuro, kata ya Komolo, wilaya ya Simanjiro, maisha yanaonekana kuwa na changamoto ya aina yake ukosefu wa mtandao wa simu. Ili waweze kupiga simu, wakazi wa hapa wanalazimika kutafuta sehemu yenye mtandao, mara nyingi wakipanda juu ya miti au kusimama maeneo ya juu.
Wananchi wanajikusanya chini ya miti na kujaribu kupandisha simu zao juu ili kupata hata chembe ya mtandao, iwe ni kwa kuwasiliana na wapendwa wao au kwa mahitaji mengine ya msingi.
Katika ulimwengu wa sasa ambapo intaneti na mawasiliano ya simu ni sehemu muhimu ya maisha, wakazi wa Sukuro wanajikuta wakiwa katika mazingira magumu. Kwao, sio jambo la kuchukua simu na kupiga, ni lazima wawe wabunifu na wavumilivu siyo kupiga picha, bali kupiga simu kwa tabu nyingi.
Tulia na sisi tutakusafirisha uone namna maisha yanavyokwenda Bila mtandao wa simu!!!!!