HATUPIGI PICHA, TUNAPIGA SIMU: Changamoto za Mawasiliano Kijijini Sukuro

Je, umewahi kufikiria maisha ambayo kila unapohitaji kuwasiliana na familia yako, ni lazima upande juu ya mti ili upate mtandao?

Katika kijiji cha Sukuro, kilichopo kata ya Komolo, wilaya ya Simanjiro, mawasiliano ya simu si jambo rahisi. Kila siku, wananchi wa kijiji hiki wanapambana na changamoto ya mtandao hafifu wa simu, hali inayowalazimu kupanda juu ya miti ili kupiga simu au kutuma ujumbe. Katika sehemu nyingine, huduma za kutuma na kupokea pesa, ambazo zinahitaji mtandao, zimegeuka kuwa safari hatari, kwani wakala wa huduma hiyo hulazimika kupanda juu ya mti ili kuhudumia wateja wake.

Kwa wakazi wa Sukuro, mawasiliano yamekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo na usalama. Wakazi, wanaelezea jinsi wanavyolazimika kutumia mbinu za kizamani na zenye hatari ili kufanikisha mawasiliano yao na ndugu zao walioko mbali.

https://www.instagram.com/reel/DA8BeY0PWDt/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Katika mazungumzo chini ya mti ambao ni sehemu pekee inayopatikana mtandao, wakazi wa kijiji hiki wameelezea hali yao kwa uchungu, wakionyesha matumaini ya kuwa siku moja, suluhisho la kudumu litapatikana. Mtendaji wa kijiji ameeleza hatua ambazo serikali ya kijiji imejaribu kuchukua ili kutafuta msaada wa kiteknolojia na kufanikisha upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika kwa wananchi.

Related Posts

TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

Serikali za vijiji katika Tarafa ya Terrat, wilayani Simanjiro, zimetakiwa kuwa na ushirikiano mzuri na wawekezaji waliopo kwenye maeneo yao kwa kuwaalika na kuwatembelea ili kujenga mahusiano mazuri na kushirikiana…

Continue reading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

Maji Safi na Salama ni Yapi?

Maji Safi na Salama ni Yapi?

Mbinu Bora za Uhifadhi wa Mazao ya Chakula kwa Usalama na Ufanisi

Mbinu Bora za Uhifadhi wa Mazao ya Chakula kwa Usalama na Ufanisi

Usalama wa Vijana Wanaochunga Mifugo Kwakuchinja

Usalama wa Vijana Wanaochunga Mifugo Kwakuchinja

Migogoro baina ya Wanyamapori na Binadamu Tanzania: Chanzo na Suluhisho

Migogoro baina ya Wanyamapori na Binadamu Tanzania: Chanzo na Suluhisho

Namna Shule ya Msingi Burunge Inavyonufaika na Uhifadhi wa Ushoroba wa Kwakuchinja

Namna Shule ya Msingi Burunge Inavyonufaika na Uhifadhi wa Ushoroba wa Kwakuchinja
Enable Notifications OK No thanks