Wadau Waunganisha Nguvu Kulinda Uoto wa Maasai Steppe

Picha ya moja ya mimea vamizi katika ukanda wa Maasai Steppe ambalo haliliki na mifugo na linazuia majani mengine kumea (Picha na Isack Dickson).

“Kwakweli ushirikiano huu ni muhimu sana kwani sisi wafugaji bila kuwa na mazingira bora, maisha yetu na mifugo yetu yatakuwa hatarini. Pia kwa kushirikiana tutaweza kupata fedha zaidi kutoka kwa wafadhili na kutumia rasilimali zetu kwa ufanisi zaidi kufikia maeneo mengi ndani ya ukanda wetu wa Maasai Steppe.”Paulo Oleleitura

Na Dorcas Charles.

Katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira katika ukanda wa Maasai Steppe, wadau kutoka mashirika mbalimbali wamekutana kujadili namna ya kuunganisha nguvu katika kulinda na kurejesha uoto wa asili.

Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni katika Wilaya ya Simanjiro, uliandaliwa na Tanzania Conservation and Community Empowerment Initiative (TACCEI) kwa kushirikiana na GLFx Maasai Steppe, na kuhudhuriwa na wadau kutoka Wilaya za Kiteto, Simanjiro, Monduli, na Longido.

Joshua Daniel Laizer, muanzilishi mwenza wa GLFx Maasai Steppe na TACCEI, amesema mkutano huo ni hatua muhimu katika kuhamasisha ushirikiano miongoni mwa wadau ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori, kupambana na mmomonyoko wa udongo, pamoja na kurejesha uoto wa asili katika ukanda huo muhimu wa malisho.

Akifafanua kuhusu mkakati huo wa ushirikiano, Joshua amesema:

Sauti ya Joshua Daniel Laizer, muanzilishi mwenza wa GLFx Maasai Steppe na TACCEI.

Aidha, Joshua ameongeza kuwa ushirikiano huu utasaidia kila shirika kufahamu wajibu wake na kuelekeza nguvu zake pale panapohitajika zaidi ili kuboresha maisha ya wananchi, hasa jamii za kifugaji zinazoishi katika eneo hili ambalo limekuwa likikabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira.

Kwa upande wake, Lidya Sanago ambaye ni Afisa wa Jinsia kutoka Enduata Community Initiative Organization, amepongeza ushirikiano huo na kusisitiza umuhimu wa vijana kuhusishwa kikamilifu katika miradi ya uhifadhi wa mazingira na urejeshwaji wa uoto wa asili. Lidya amesema:

Sauti ya Lidya Sanago Afisa wa Jinsia kutoka Enduata Community Initiative Organization.

Naye Paulo Oleleitura, Mkurugenzi wa shirika la Mulika Afrika, lenye malengo ya kuboresha afya, elimu, na mazingira amesema kuwa ushirikiano huu ni wa muhimu mno kwa jamii za kifugaji kwani mafanikio ya uhifadhi wa mazingira yana uhusiano wa moja kwa moja na ustawi wa maisha yao. Paulo amesema:

Sauti ya Paulo Oleleitura, Mkurugenzi wa shirika la Mulika Afrika.

Wadau hawa pia wametoa wito kwa serikali kuweka mazingira rafiki na sera zitakazoruhusu jamii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira, kwani wao ndio wahusika wakuu katika matumizi ya rasilimali hizo.

Ushirikiano huu unatarajiwa kuleta mafanikio makubwa katika uhifadhi na urejeshaji wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kuongeza ustawi wa jamii za kifugaji katika ukanda mzima wa Maasai Steppe.

Related Posts

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria ili kudhibiti ajali kutokana na ongezeko la wasafiri kipindi cha likizo za shule. Madereva wamehimizwa kuzingatia sheria…

Continue reading
Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Zaidi ya madereva 800 wa magari ya utalii mkoani Arusha wamepatiwa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ikiwa ni maandalizi ya msimu wa utalii (high…

Continue reading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

Madereva wa Serikali Arusha Wawezeshwa kwa Mafunzo ya Usalama Barabarani

Madereva wa Serikali Arusha Wawezeshwa kwa Mafunzo ya Usalama Barabarani

Wadau Waungana Kunusuru Mazingira ya Maasai Steppe

Wadau Waungana Kunusuru Mazingira ya Maasai Steppe
Enable Notifications OK No thanks