“Kutokana na kipato kidogo vijana hawana hela za kuweza kuwawezesha kwenye michakato ya uchaguzi” Kijana.
Na Dorcas Charles.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 vijana ni asilimia 46. Tafsiri ya kijana inasema kijana ni yule mwenye umri wa miaka 15 hadi 35
Sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2019 inataka ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika ngazi zote za maamuzi mjini na vijijini
mkakati wa sera ya vijana umeainisha bayana majukumu ya kila mdau katika kufanikisha sera ya maendeleo ya vijana ili kufikia malengo ya kuwawezesha vijana nchini katika nyanja za kiuchumi ,kijamii na kisiasa
Lakini jee malengo haya yanaakisi na sera inavyoseama, Vijana wanaeleza nini kinapelekea wao kutokushika nafasi za uongozi?
Inatambulika kuwa vijana ndio wenye nguvu , wazalishaji na wakati mwengine enye ubunifu na afya na ni kundi kubwa lililopo katika jamii swali la kujiuliza wanaaminika katika kushika nafasi za uongozi, baadhi ya wazee wa mtaa wa mita 200 kata ya Ngarenaro mkoani Arusha wanaeleza.
Ili kuhakikisha masuala yanayowakabili vijana yanashuhulikiwa ni muhimu kuwa na makakati wa kuwashirikisha vijana katika mchakato wa maamuzi na majukumu ya uongozi na kuwaandaa vijana katika nafasi za uongozi.
Wenyekiti wa mtaa wa Mita mia mbili Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha Peter Lukumay anasema wao wanawaanda vjana kushika nafasi za uongozi.
Ili vijana wengi kujitokeza kuwania nafasi za uongozi katika chaguzi zote za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu nini kifanyike, vijana hawa na mwenyekiti wa kijiji cha mita 200 wanaeleza.