Wanawake na Uongozi: Je, Mikutano ya Viongozi Inawapa Nafasi ya Kujadili Fursa za Uongozi?

Na Dorcas Charles.

Katika jamii nyingi nchini Tanzania, mila na desturi zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wanawake kushiriki katika maamuzi ya uongozi. Hali hii inawanyima nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Ingawa juhudi mbalimbali zinafanywa kuhakikisha usawa wa kijinsia, bado kuna changamoto zinazowafanya wanawake wasijitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi.

Katika mikutano ya viongozi, wanawake wanapata nafasi ya kuzungumza lakini bado wapo wanaoona hofu ya kujitokeza au kushiriki kwa ujasiri. Baadhi ya wananchi wanasema kuwa hata pale wanapoitwa kushiriki, wanawake wengi hujizuia kwa kuhisi kuwa si nafasi yao kujihusisha na maamuzi makubwa ya kijamii. Mmoja wa wananchi alisema, “Wanawake kwenye mikutano wakiitwa wanapewa fursa lakini wakati mwingine wao wenyewe ndiyo wanaogopa.” Hali hii inaonesha kuwa bado kuna kazi kubwa ya kuhakikisha wanawake wanahamasishwa na kupewa ujasiri wa kushiriki kikamilifu katika mijadala ya maendeleo na nafasi za uongozi.

Tatizo hili lina mizizi yake katika mila na desturi zilizokita mizizi kwa muda mrefu. Katika jamii ya Wamaasai, kwa mfano, wanawake kwa muda mrefu wamekuwa wakichukuliwa kama walezi wa familia pekee na si watu wa kushiriki katika maamuzi makubwa ya kijamii. Haki ya kijinsia bado ni changamoto kwa sababu wanawake wengi hawana mamlaka katika maamuzi, na nafasi zao zimeendelea kuwa finyu katika nyanja za kisiasa na kiutawala. Afisa Tarafa wa Kiruswa anasema kuwa ili kufanikisha usawa wa kijinsia, ni muhimu wanawake wapate elimu kwa wingi kwani wengi wao bado hawajahitimu masomo ili kuwa na ujasiri wa kuwania nafasi za uongozi.

Elimu ni silaha muhimu katika mapambano haya, lakini bado wanawake wengi wanakosa fursa za kielimu kutokana na changamoto za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Hali ya kiuchumi pia inachangia kwa kiasi kikubwa kwani wanawake wengi wanakosa rasilimali za kifedha za kuwawezesha kushiriki katika siasa au hata kuendesha kampeni za uchaguzi.

Wanaopata elimu nao hukutana na changamoto ya kukubalika katika jamii zao, hasa pale wanapoonyesha nia ya kuwania nafasi za uongozi,Afisa tarafa wa tarafa ya Terrat Bwana Lekshon Kiruswa anafafanua zaidi akieleza kuwa serikali inatoa nafasi sawa lakini anaanza kwa kueleza maana haswa ya Usawa wa kijinsia.

Ripoti ya Tanzania Gender Indicators (2023) inaonyesha kuwa bado kuna uwiano mkubwa kati ya wanaume na wanawake katika nafasi za uongozi, ambapo wanawake wanawakilishwa kwa chini ya asilimia 30 katika baadhi ya ngazi za uongozi wa vijiji na kata. Hali hii inaonyesha kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanikisha usawa wa kijinsia.

Viongozi wa jamii na taasisi mbalimbali wanapaswa kuhakikisha kuwa wanawake wanahamasishwa kwa njia zote ili wawe na ujasiri wa kushiriki katika uongozi. Kampeni za kuwaelimisha wanawake kuhusu haki zao na umuhimu wa ushiriki wao katika siasa na uongozi zinapaswa kuongezeka. Viongozi wa mila pia wanapaswa kushirikishwa katika mabadiliko haya kwa kuwa wao ni sehemu muhimu ya mfumo wa kijamii unaoathiri maisha ya wanawake wengi.

  • Related Posts

    Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

    Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria ili kudhibiti ajali kutokana na ongezeko la wasafiri kipindi cha likizo za shule. Madereva wamehimizwa kuzingatia sheria…

    Continue reading
    Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

    Zaidi ya madereva 800 wa magari ya utalii mkoani Arusha wamepatiwa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ikiwa ni maandalizi ya msimu wa utalii (high…

    Continue reading

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *

    You Missed

    Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

    Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

    Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

    Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

    Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

    Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

    Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

    Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

    Madereva wa Serikali Arusha Wawezeshwa kwa Mafunzo ya Usalama Barabarani

    Madereva wa Serikali Arusha Wawezeshwa kwa Mafunzo ya Usalama Barabarani

    Wadau Waungana Kunusuru Mazingira ya Maasai Steppe

    Wadau Waungana Kunusuru Mazingira ya Maasai Steppe
    Enable Notifications OK No thanks