
Simanjiro ni mojawapo ya wilaya zinazokumbwa na changamoto kubwa ya ukame, hali inayochangia uhaba wa maji safi na salama kwa wakazi wake. Ukame huu umeathiri kwa kiasi kikubwa vyanzo vya maji, na hivyo kuathiri maisha ya jamii za wafugaji na wakulima.
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2022, zaidi ya mifugo 92,000 ilipoteza maisha kutokana na ukosefu wa maji. Hali hii imewaathiri kwa kiasi kikubwa wafugaji wa Kimasai, ambao wanategemea mifugo kwa ajili ya kipato na chakula.
Maji Safi na Salama ni Nini?
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), maji safi na salama ni yale yanayokidhi viwango vya ubora wa maji kwa matumizi ya binadamu. Maji haya yanapaswa kuwa salama kwa kunywa, kupika, kuoga, na matumizi mengine ya nyumbani bila kuhatarisha afya ya binadamu.
Hata hivyo, kwa wakazi wa Simanjiro, upatikanaji wa maji yenye ubora huo bado ni changamoto. Wakazi wengi hutegemea mabwawa, visima virefu, na maji ya mvua, ambayo mara nyingi hayakidhi viwango vya usalama wa afya.
Upatikanaji wa maji safi na salama ni haki ya msingi ya kila mwanadamu. Kwa wilaya ya Simanjiro, bado kuna safari ndefu ya kuhakikisha kila mkazi anapata maji safi kwa matumizi ya kila siku.
Ili kusikiliza makala hii kwa njia ya sauti hapa chini.