
Shirika la KINNAPA Tanzania limeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii za wafugaji, wakulima wadogo, waokota matunda, na makundi ya pembezoni kote nchini Tanzania, kwa kutoa elimu, huduma za afya, maji safi, usafi wa mazingira, pamoja na kuendeleza uhifadhi wa mazingira ya asili.
Akizungumza kuhusu shughuli hizo, Mkurugenzi wa shirika hilo, Paulina Peter Ngurumwa, amesema KINNAPA inalenga kuinua wanawake na wasichana kupitia elimu na ujasiriamali, ikiwa ni sehemu ya kukuza maendeleo jumuishi na usawa wa kijinsia katika jamii za vijijini.
Aidha, amesema mafanikio hayo yanatokana na juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali kama KINNAPA, ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha haki za binadamu, usawa wa kijinsia na maendeleo shirikishi.
Jamii Yaona Mabadiliko
Wakati huo huo, wananchi waliotoa maoni kupitia makundi ya kijamii na mikutano ya hadhara wameeleza kuwa wanawake kwa sasa wanaamka na kutambua haki zao. Amos Levando, mkazi wa Arusha, alisema:
Conjesia Peter Mushi, mwanaharakati wa maendeleo ya wanawake, alisisitiza umuhimu wa wanawake walioelimika kurudisha maarifa yao kwa jamii:
KINNAPA: Kazi Zaidi ya Maneno
Pamoja na kuwa na makao yake makuu wilayani Babati mkoani Manyara, shirika la KINNAPA limekuwa likitekeleza miradi katika mikoa mbalimbali nchini, likifanya kazi bega kwa bega na serikali, mashirika mengine, na jamii husika kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika maendeleo.
Kwa kutumia mbinu jumuishi, shirika hilo linaweka mkazo katika nyanja za:
- Elimu ya kijamii na haki za binadamu
- Uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana
- Uhifadhi wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali asilia
- Afya ya msingi na usafi wa mazingira
Katika zama hizi za mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, KINNAPA linaendelea kuwa sauti ya matumaini kwa wanawake na wasichana wanaojitokeza kudai nafasi yao katika ujenzi wa taifa.