Mkuu wa Wilaya Monduli Aahidi Kulinda Ardhi ya Malisho Mswakini

Na Nyangusi Ole Sang’ida

Tarehe 17 Aprili 2025, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Festo Kiswaga, alifanya ziara ya kikazi katika kata ya Mswakini ili kusikiliza kero za wananchi na kushughulikia changamoto za ardhi. Katika ziara hiyo, Mhe. Kiswaga aliwahakikishia wakazi wa Mswakini kuwa ardhi yao ya malisho italindwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo, akisisitiza umuhimu wa kulinda rasilimali za jamii.

Mhe. Kiswaga aliwaasa wananchi kuvutia wawekezaji wa utalii, akibainisha kuwa eneo la Mswakini, lililo karibu na hifadhi ya wanyama na Ziwa, lina uwezo mkubwa wa kiuchumi. “yaani ninyi mpo katikati ya pesa,fanyeni hivyo ili mumsaidie Rais kuongeza idadi ya watalii” alisema. Aidha, aliwataka wakazi wasikae kimya wanaposhuhudia vitendo vya kuuza ardhi bila ridhaa yao, akisema, “Pigeni kelele..Tumieni huu ushauri mtakuja kunishukuru.”

Katika hatua ya maana, Mhe. Kiswaga alifanikisha kumaliza mgogoro wa ardhi uliokuwa unatishia amani Mswakini. Tume iliyoundwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ilichunguza suala hilo na kutoa mapendekezo yaliyosababisha kurejeshwa kwa eneo la malisho lililovamiwa. “Eneo lililozidi lizrudi kwenye serikali ya kijiji,” alisema Kiswaga.

Ziara hii inaonyesha dhamira ya Mhe. Kiswaga ya kuhakikisha haki za wananchi wa Monduli zinazingatiwa, hasa katika masuala ya ardhi. Kwa wale wanaotaka kufuatilia masuala ya ardhi na maendeleo Monduli, endelea kushikamana nasi kwa habari zaidi.

Related Posts

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la madiwani jiji la Arusha limefungwa rasmi katika hafla ya kipekee iliyoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Mohamed Mchechengerwa.…

Continue reading
Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

World Sickle Cell Awareness Day ni siku inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Juni ili kuhamasisha elimu juu ya ugonjwa wa sikoseli. Ugonjwa huu wa damu, unaosababisha mabadiliko ya seli nyekundu…

Continue reading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa
Enable Notifications OK No thanks