WAZIRI MKUU AWATAKA WAHANDISI WAZINGATIE MAADILI

#Habari WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa awataka wahandisi wote nchini wazingatie miiko na maadili ya taalum hiyo ikiwemo kuitekeleza miradi ya ujenzi kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha halisi iliyotolewa.

“Sote tunatambua kwamba wapo wachache katika taaluma yenu ya uhandisi ambao wanaichafua kwa kufanya matendo ambayo ni kinyume na taaluma lakini pia ni kinyume na maadili.” “Matendo hayo ni pamoja na rushwa, ubadhilifu, na ukosefu wa weledi. Hii si tu kwamba inachafua taaluma ya uhandisi, bali pia inaharibu taswira ya nchi”.

Ameyasena hayo leo (Desemba 06, 2024) kwenye Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Bodi ya usajili wa Wahandisi isimamie maadili ya kihandisi na makampuni ya kihandisi kwa mujibu wa sheria ili kulinda hadhi ya uhandisi nchini.

Waziri Mkuu ametoa rai kwa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) kuendelea kushirikiana na vyombo mbalimbali kuwabaini wanaokiuka maadili na sheria na kuchukua hatua stahiki kwani taaluma ya uhandisi ni muhimu na inapaswa kutunza na kulinda heshima yake.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mita na Usalama Barabarani kuhakikisha kuwa vizuizi na vituo vya ukaguzi vinazingatia usalama wa watumiaji na tahadhari zote za kiusalama.

“Wahandisi na wataalamu wetu mnao wajibu wa kuendelea kubuni na kupendekeza mifumo bora ya alama za barabarani, usimamizi wa miundombinu ya barabarana uwekaji wa vituo vya ukaguzi ili kupunguza ajali na madhara yake.”

  • Related Posts

    WAZIRI NDEJEMBI: WATHAMINI, HAKIKISHENI THAMANI HALISI INAJULIKANA

    #Habari Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Deogratius Ndejembi amewataka Wathamini nchini kupunguza migogoro inayotokana na uthamini kwa kuhakikisha thamani halisi ya ardhi inayofanyiwa uthamini inajulikana.    Ndejembi…

    Continue reading

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *

    You Missed

    TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

    TAWA Yasihi Serikali za Vijiji Kwenye Uhifadhi Kuimarisha Ujirani Mwema na Wawekezaji

    Maji Safi na Salama ni Yapi?

    Maji Safi na Salama ni Yapi?

    Mbinu Bora za Uhifadhi wa Mazao ya Chakula kwa Usalama na Ufanisi

    Mbinu Bora za Uhifadhi wa Mazao ya Chakula kwa Usalama na Ufanisi

    Usalama wa Vijana Wanaochunga Mifugo Kwakuchinja

    Usalama wa Vijana Wanaochunga Mifugo Kwakuchinja

    Migogoro baina ya Wanyamapori na Binadamu Tanzania: Chanzo na Suluhisho

    Migogoro baina ya Wanyamapori na Binadamu Tanzania: Chanzo na Suluhisho

    Namna Shule ya Msingi Burunge Inavyonufaika na Uhifadhi wa Ushoroba wa Kwakuchinja

    Namna Shule ya Msingi Burunge Inavyonufaika na Uhifadhi wa Ushoroba wa Kwakuchinja
    Enable Notifications OK No thanks