![](https://ors-radio.co.tz/wp-content/uploads/2024/07/oip-1.jpeg)
Na Dorcas Charles.
Wananchi wameshauriwa kutumia choo bora ili kujiepusha na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu, homa ya matumbo na magonjwa mengine yanayosbabishwa na uchavuzi wa mazingira.
Ushauri huo umetolewa na mganga mfawidhi wa kituo cha afya Terrati dokta Amiri Ridhiwani Amiri wakati akifanya mahojiano na mwandishi wetu Dorcas Charles akianza kwa kueleza madhara yatokanayo na kutotumia choo bora.