Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Disemba 29, 2024, ametembelea na kutoa zawadi za sikukuu ya mwaka mpya 2025 katika vituo vitatu vya watu wenye mahitaji maalum vilivyopo wilayani Babati. Vituo hivyo ni:
- Kituo cha Kulelea Wazee Magugu
- Kituo cha Kulelea Watoto Wenye Ulemavu Unaotibika cha Zilper
- Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wanaoishi Mazingira Magumu cha Hossana
Zawadi hizo zimetolewa kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama ishara ya upendo wake kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu wakati wa sikukuu hizi.
Mhe. RC Sendiga alieleza kuwa zawadi zilizotolewa, zenye thamani ya Shilingi Milioni 6.5, ni pamoja na:
- Mchele
- Mafuta ya kupikia
- Sukari
- Unga wa ngano
- Viungo
- Sabuni
- Juisi
- Maji
- Mbuzi
Amesema kuwa zoezi la ugawaji zawadi linaendelea katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara, lengo likiwa ni kuwafariji na kushirikiana na makundi maalum katika jamii.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwahimiza wananchi kuendelea kuonyesha mshikamano, upendo, na kushirikiana na makundi haya maalum ili kudumisha mshikamano wa kijamii.