
Katika kipindi cha kiangazi, wakazi wa Kijiji cha Terrat hukumbwa na changamoto ya upatikanaji wa mboga za majani. Hata hivyo, hali hii pia inatoa fursa kwa wakulima wabunifu wanaotumia mbinu mbalimbali kuzalisha mboga na kupata kipato.
Katika makala hii, mwanahabari Evander Barnaba anazungumza na mama anayejipatia kipato kupitia kilimo cha mboga mboga licha ya changamoto ya upatikanaji wa maji ya umwagiliaji. Pamoja na vikwazo hivyo, anaendelea kupambana kuhakikisha anazalisha mazao ya kutosha kwa ajili ya familia yake na jamii inayomzunguka.
Sikiliza makala ya sauti kwa undani zaidi kwa kubofya hapa chini.