
Katika kukabiliana na changamoto kubwa za kimazingira zinazoathiri ukanda wa Maasai Steppe (Kiteto, Simanjiro, Monduli na Longido), wadau mbalimbali wamekutana Simanjiro kujadili mikakati ya pamoja ya kurejesha uoto wa asili. Wakizungumza wakati wa warsha iliyoandaliwa na mtandao wa GLFx Maasai Steppe na TACCEI, wadau wamehimiza ushiriki wa jamii, hasa vijana, katika kulinda mazingira na kuimarisha uchumi wa jamii za kifugaji.
Sikiliza habari kamili iliyoambatana na sauti za wadau mbalimbali hapa chini.