![](https://ors-radio.co.tz/wp-content/uploads/2024/06/migogoro-pic.jpg)
Changamoto ya migogoro kati ya wanyamapori na binadamu inazidi kuongezeka Tanzania, hasa kwa jamii zilizo karibu na hifadhi na mapito ya wanyama. Taarifa zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2012 na 2019, zaidi ya watu 1,069 walipoteza maisha kutokana na migogoro hii, huku mazao yenye thamani ya mamilioni ya fedha yakiharibiwa.
Tatizo hili linatokana na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ongezeko la makazi ya binadamu karibu na maeneo ya wanyamapori, kilimo kisicho endelevu, na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Wakazi wa vijiji kama Mswakini Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wameeleza jinsi wanyama kama tembo wanavyoharibu mazao na kusababisha hofu miongoni mwa jamii.
![](https://ors-radio.co.tz/wp-content/uploads/2024/01/MGOGOROO.jpg)
Serikali na wadau wa uhifadhi wanaendelea kutafuta suluhisho kupitia miradi ya elimu kwa jamii, ujenzi wa uzio wa umeme, na mipango ya matumizi bora ya ardhi. Pia, jitihada za kurudisha mapito ya wanyama na kupunguza ujangili zinaendelea kutekelezwa.
Sikiliza makala hii maalumu kuhusu Migogoro baina ya wanyamapori na binadamu nini chanzo?