MRADI MPYA WA TEKNOLOJIA KUBORESHA AFYA YA MIFUGO SIMANJIRO

Katika jitihada za kuboresha afya ya mifugo, hususan mbuzi na kondoo, wataalamu wa mifugo kutoka Wilaya ya Simanjiro wamekutana leo katika ukumbi wa mikutano wa Ilaramata (Manyara Hall) kujadili mradi mpya wa afya ya mifugo. Mradi huu unafadhiliwa na Chuo Kikuu cha Glasgow, Uingereza, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), na unalenga kutumia app ya simu kusaidia watoa huduma ngazi ya jamii.

Dkt. Yassin Mshana, mtaalamu wa mifugo kutoka idara ya Mifugo, Kilimo, na Uvuvi Wilaya ya Simanjiro, amesema kuwa “app hii itawezesha wahudumu wa afya ya mifugo kutambua magonjwa kwa urahisi na kupata mwongozo wa tiba sahihi.” App hiyo itakuwa suluhisho kwa changamoto ya kutofahamu magonjwa yanayoathiri wanyama wadogo na pia kusaidia mawasiliano kati ya watoa huduma na wataalamu wa mifugo.

Mmoja wa wataalamu wa mifugo, Tila Shinini, ameongeza kuwa mara nyingi wahudumu wa jamii wanakabiliwa na changamoto ya kutambua magonjwa sahihi kutokana na dalili zinazofanana, lakini kupitia app hii, “wahudumu wataweza kuingiza dalili walizoziona kwa mifugo, na mfumo wa app utawasaidia kupata majibu sahihi na ushauri wa tiba.

Changamoto nyingine kubwa iliyobainishwa na wahudumu wa mifugo ni ukosefu wa mtandao wa mawasiliano na usafiri wa kuwafikia wafugaji kwa wakati. Mara nyingi, wahudumu wanakosa mafuta ya pikipiki au kushindwa kuwasiliana na wataalamu wa mifugo. “App hii itasaidia kupunguza changamoto hizi kwa kuwezesha utambuzi wa magonjwa hata bila mawasiliano ya moja kwa moja na daktari wa mifugo.”

Wadau wa mifugo wamepongeza mradi huu na kupendekeza kuwa ili kufanikisha utekelezaji wake kwa ufanisi zaidi, app itafsiriwe kwa Kiswahili ili iwe rahisi kutumiwa na wahudumu wa jamii. Pia, wameomba kuwepo na mafunzo maalum kwa watoa huduma ili kuhakikisha wanaelewa matumizi ya app hii kikamilifu.

Mradi huu unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya afya ya mifugo Simanjiro na kusaidia wafugaji kupata huduma bora kwa wanyama wao, kupunguza vifo vya mifugo, na kuongeza uzalishaji wa mifugo kwa jamii ya wafugaji.

Related Posts

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la madiwani jiji la Arusha limefungwa rasmi katika hafla ya kipekee iliyoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Mohamed Mchechengerwa.…

Continue reading
Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

World Sickle Cell Awareness Day ni siku inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Juni ili kuhamasisha elimu juu ya ugonjwa wa sikoseli. Ugonjwa huu wa damu, unaosababisha mabadiliko ya seli nyekundu…

Continue reading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa
Enable Notifications OK No thanks