Mbwa Wakali Waua Mifugo, Wajeruhi Watoto

Nyangusi Ole Sang’ida

Ilkirevi, Arusha – Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilkirevi kilichopo katika Kata ya Olturoto, Wilaya ya Arusha, Bw. Abraham Gerald Mollel ameongoza operesheni ya kijiji dhidi ya mbwa wakali waliowavamia na kuwadhuru binadamu pamoja na mifugo.

Katika tukio hilo la aina yake, mbwa zaidi ya 13 wameripotiwa kuvamia vitongoji vya Olturoto na Oloirowa, ambapo wamesababisha majeraha kwa mtoto mdogo wa miaka 4, kuua kuku takribani 30, na kondoo 6. Mzee mmoja alijeruhiwa kwa kung’atwa mguu. Msako uliohusisha vijana wa kijiji umefanikiwa kuwaua mbwa kati ya 6 hadi 8 hadi sasa.

Mwenyekiti Mollel amesema kuwa licha ya kutokuwa na sheria inayoruhusu moja kwa moja kuuawa kwa mbwa, hatua hiyo imelenga kulinda maisha ya binadamu na mifugo. Aidha, alisisitiza kuwa wamiliki wa mbwa waliowashambulia watu watafikishwa mahakamani.

“Fuga kwa starehe zako, lakini ukiwaachia wahatarishe watu, lazima utaitwa kujibu,” alisema Mollel.

Mkazi jirani Gidion Lengoisai alielezea tukio hilo kama la kutisha na kusema usiku huo alisikia kelele saa 8:25 usiku, na baada ya kufuatilia alikuta mbwa wakiua mifugo ya jirani. Juhudi za haraka za wananchi zilizuia madhara zaidi.

Mwenyekiti amesema msako bado unaendelea na ametoa wito kwa wamiliki wa mbwa kuwajibika ipasavyo ili kuepusha madhara kwa jamii.

  • Related Posts

    Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

    Baraza la madiwani jiji la Arusha limefungwa rasmi katika hafla ya kipekee iliyoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Mohamed Mchechengerwa.…

    Continue reading
    Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

    World Sickle Cell Awareness Day ni siku inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Juni ili kuhamasisha elimu juu ya ugonjwa wa sikoseli. Ugonjwa huu wa damu, unaosababisha mabadiliko ya seli nyekundu…

    Continue reading

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *

    You Missed

    Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

    Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

    Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

    Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

    Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

    Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

    Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

    Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

    Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

    Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

    Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

    Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa
    Enable Notifications OK No thanks