Kampeni ya Mama Samia Yaendelea Kutoa Msaada wa Kisheria Arusha

Na Nyangusi Ole Sang’ida

Arusha, Tanzania – Wizara ya Katiba na Sheria kupitia mpango wa Mama Samia Legal Aid imeendelea kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi mkoani Arusha, ikiwa ni juhudi za kuongeza uelewa wa haki za binadamu, hususan haki za wanawake na watoto. Mpango huu pia unalenga kuimarisha huduma za ushauri wa kisheria na unasihi kwa waathirika na manusura wa ukatili wa kijinsia.

Katika kikao na waandishi wa habari, Wakili wa Serikali, Dismas, alieleza maendeleo ya msaada wa kisheria kwa wananchi na kuelezea migogoro iliyosikilizwa zaidi kupitia mpango huo.

Martha Lyimo, ambaye anahusika na masuala ya haki za wanawake na watoto, alitoa maoni yake kuhusu umuhimu wa msaada wa kisheria kwa jamii, akisisitiza namna huduma hii inavyosaidia kupunguza migogoro na kuleta suluhisho kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.

Mmoja wa wananchi waliopokea msaada wa kisheria, mfanyabiashara kutoka wilaya ya Karatu, alielezea jinsi huduma hiyo ilivyosaidia kutatua changamoto zake za kisheria.

Mpango wa Mama Samia Legal Aid unaendelea kuwa msaada mkubwa kwa jamii, ukihamasisha wananchi kujua haki zao na kupata usaidizi wa kisheria bila gharama.

Related Posts

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la madiwani jiji la Arusha limefungwa rasmi katika hafla ya kipekee iliyoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Mohamed Mchechengerwa.…

Continue reading
Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

World Sickle Cell Awareness Day ni siku inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Juni ili kuhamasisha elimu juu ya ugonjwa wa sikoseli. Ugonjwa huu wa damu, unaosababisha mabadiliko ya seli nyekundu…

Continue reading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Baraza la Madiwani Arusha Laitimishwa Rasmi, Viongozi Wasisitiza amani

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Siku ya Elimu ya Ugonjwa wa Sikoseli Duniani — 19 Juni: Kuleta Mwanga kwa Wagonjwa na Jamii

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Polisi Arusha Waimarisha Ukaguzi wa Mabasi Kukabiliana na Ajali

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Madereva 800 Wapatiwa Mafunzo Maalumu Kuelekea Msimu wa Utalii Arusha

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Kijana auawa kwa kisu Arusha, wananchi wachoma nyumba ya mtuhumiwa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa

Jamii ya Maa Iwe Makini na Wanaotaka Kuigombanisha na Serikali – Fred Lowassa
Enable Notifications OK No thanks